Senegal na Ufaransa zakubaliana kuhusu kuondoka kwa wanajeshi jijini Dakar

Mawaziri wa mambo ya nje wa Ufaransa na senegal wamekubaliana kuunda tume ya pamoja kwa ajili ya kuandaa mchakato wa kuondoka kwa viksoi vya Ufaransa nchini Senegal ifikapo mwisho wa mwaka 2025.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa yao ya pamoja nchi hizi mbili zinakusudia kufanyia kazi ushirikiano mpya wa ulinzi na usalama ambao utazingatia vipaumbele vya kimkakati vya pande zote.

Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye mwishoni mwa mwaka uliopita, alisema kwamba Ufaransa iliyokuwa mkoloni wa zamani wa Senegal inapaswa kufunga kambi zake zote za kijeshi katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi na kuondoka.

Hivi karibuni hakutakuwa na wanajeshi zaidi wa Ufaransa nchini Senegal, Faye aliliambia gazeti la Le Monde mwezi Novemba, akisisitiza umuhimu wa uhuru wa kitaifa.

Rais wa Senegal- Bassirou Diomaye Faye.
Rais wa Senegal- Bassirou Diomaye Faye. © le site officiel de la présidence du Sénégal

Jeshi la Ufaransa limedumisha uwepo wake nchini Senegal tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake mnamo 1960, haswa kwa mafunzo na operesheni za usalama za kikanda. Hivi sasa kuna wanajeshi 350 wa Ufaransa nchini humo.

Maoni ya Faye yaliashiria kauli ya kwanza kutoka kwa serikali ya Senegal iliyotaka kuondoka kwa wanajeshi wa Ufaransa.

Waziri Mkuu Ousmane Sonko alikosoa uwepo wa wanajeshi wa Ufaransa mwezi Mei alipohoji ulazima wa kuwa na taifa huru.