Senegal: Mawaziri watano wa rais wa zamani Macky Sall kufikishwa katika Mahakama Kuu ya Haki

Nchini Senegal, mawaziri watano wa zamani watahukumiwa hivi karibuni na Mahakama Kuu ya Haki. Wengi wa wabunge wa Bunge la taifa wamepiga kura siku ya Alhamisi, Mei 8, kwa azimio la kufungulia mashitaka kulingana na kanuni hizi.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Dakar, Birahim Touré

Msururu wa kesi utaanza hivi karibuni mbele ya mahakama hii maalum, ambayo ndiyo pekee iliyoidhinishwa kusikiliza kesi dhidi ya mawaziri wa zamani au wakuu wa nchi. Shutuma dhidi ya mawaziri hao zinahusiana zaidi na tuhuma za ubadhirifu wa fedha kwa kukabiliana na janga la UVIKO-19. Wote wanakabiliwa na tuhuma hiyo isipokuwa waziri wa zamani wa sheria, ambaye anatuhumiwa kwa ufisadi.

Moustapha Diop, Amadou Mansour Faye, Aissatou Sophie Gladima, Salimata Diop na Ismaïla Madior Fall, mawaziri wote wa zamani waliohudumu chini ya Macky Sall, wanaunda kundi la kwanza la mawaziri wa zamani ambao watafikishwa mbele ya Mahakama Kuu ya Haki. Huu ndio ulikuwa uamuzi wa Bunge la taifa, ambalo limepiga kura siku ya Alhamisi alasiri juu ya maazimio yakuwafungulia mashitaka ili kutoa mwanga juu ya usimamizi wa fedha zilizotengwa kwa vita dhidi ya coronavirus.

Sehemu ya hazina hii ya “force Covid-19”, iliyokusudiwa kusaidia kaya na kampuni ziliokuwa katika matatizo wakati wa janga hili, iliripotiwa kuelekezwa kinyume. Kulingana na ripoti ya Mahakama ya Wakaguzi wa Hesabu ya mwaka 2023, ambayo iliifanya ofisi ya mwendesha mashtaka wa fedha ya Dakar katikati ya mwezi wa Aprili kutangaza nia yake ya kuwashtaki watu kadhaa, wakiwemo mawaziri wa zamani.

Mahakama imeombwa mara mbili pekee tangu 1960

Kwa hivyo, wabunge wengi wameamua kuidhinisha mahakama ili kutoa mwanga juu ya madai haya ya ubadhirifu. Kati ya mawaziri hao watano, ni Waziri wa zamani wa sheria pekee ndiye anayeshitakiwa kwa kesi isiyohusiana na Uviko-19. Ismaïla Madior Fall anatuhumiwa kwa ubadhirifu na ufisadi, miongoni mwa mambo mengine.

Tangu mwaka 1960, Mahakama Kuu ya Haki imeombwa mara mbili tu. Mnamo mwaka 1963 kwa kumuhukumu rais wa zamani wa Baraza Mamadou Dia na mnamo mwaka 2005 kwa Waziri Mkuu wa zamani Idrissa Seck ambaye hatimaye alifukuzwa kazi kabisa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *