Selcom yazindua vituo 10 vya Huduma kwa Wateja: Kuweka pesa Selcom Pesa na wakala sasa ni rahisi

Dar es Salaam. Kampuni ya huduma za kifedha ya  Selcom Tanzania, imetangaza uzinduzi rasmi wa vituo vipya 10 vya Selcom Experience Centers jijini Dar es Salaam, vyenye lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za Selcom kwa urahisi, ikiwemo upatikanaji wa ‘float’ kwa mawakala wa Selcom pamoja na kuwezesha wateja wa Selcom Pesa kuongeza pesa kwenye akaunti zao kwa haraka, salama, na bila gharama ya ziada.

Kupitia vituo hivi, mawakala wa Selcom  sasa wana uwezo wa kupata float kwa urahisi zaidi kuliko awali, jambo linalowawezesha kutoa huduma kwa ufanisi.

Wakati huo huo, wateja wa Selcom Pesa wanaweza kufika katika vituo hivyo kuongeza pesa kwenye akaunti zao papo hapo, kupata kadi ya Mastercard, na kupewa msaada wa moja kwa moja kuhusu matumizi ya huduma nyingi zilizopo kwenye Selcom Pesa.

Meneja vituo vya Selcom Experience centers akielezea huduma zinazopatikana katika vituo vipya vya Selcom.

Wateja hawalazimiki kufika kwenye kituo kufungua akaunti ya Selcom Pesa yenye Makato Madogo Kuliko huduma zingine, wanaweza kupakua aplikesheni kwenye Play Store au App Store usajil unafanyika moja kwa moja kupitia simu kwa kutumia namba ya NIDA.

Hata hivyo, vituo hivi vimeboreshwa kuwa sehemu muhimu ya huduma kwa wateja wanaohitaji msaada wa moja kwa moja, elimu juu ya huduma, au wanaotaka kuwa sehemu ya mtandao wa Selcom kama mawakala.

Usajili wa uwakala, upatikanaji wa POS mashine na roller, huduma za duka direct na maelezo muhimu kuhusu Selcom hutolewa katika kila kituo.

Kituo cha Selcom Experience Center Mbagala Zakhiem.

Vituo vya Selcom Experience Centers vinapatikana katika maeneo ya Gongo la Mboto (Mtaa wa Banana), Manzese, Mbagala (Zakhem), Tabata Kinyerezi, Mbezi Mwisho Luis, Mbezi Tanki Bovu, Mwenge, Masaki, Kariakoo (Mtaa wa Uhuru na Nyamwezi) na Jamhuri Posta.

Vituo hivi vimewekewa timu mahiri ya huduma kwa wateja na miundombinu inayowezesha utoaji wa huduma bora kwa wakati wote. Vituo vinafunguliwa kuanzia saa 2 Asubuhi mpaka saa 2 usiku, siku za Jumatatu mpaka Jumamosi, na saa 2 Asubuhi mpaka 11 jioni siku ya Jumapili.

Kwa kutumia aplikesheni ya Selcom Pesa, wateja wanaweza kutuma na kupokea fedha, kulipia huduma za taasisi mbalimbali na kufanya miamala kwa makato madogo kuliko huduma nyingine, unafuu wa hadi asilimia 60 chini ya viwango vya watoa huduma wengine.

Kituo cha Selcom Experience center Mazense.

Unaweza kupakua aplikesheni ya Selcom Pesa kutoka kwenye simu zote za Android au Iphone na kujisajili mwenyewe, kinachohitajika ni NIDA namba pekee, au unaweza kutumia USSD code *150*35# kwa simu za kawaida (Kiswaswadu).

Selcom pia imethibitisha kuwa uzinduzi huu ni hatua ya kwanza katika mkakati mpana wa kupanua vituo vya huduma katika maeneo mengine ya Dar es Salaam na mikoa mbalimbali nchini, ndani ya mwaka huu. Kupitia mpango huu, Selcom inalenga kuimarisha ujumuishaji wa kifedha na kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma ya kifedha iliyo salama, nafuu, na inayopatikana kwa urahisi.

Kwa maelezo zaidi kuhusu maeneo ya vituo tembelea tovuti https:// www.selcom.net/selcomcontactus  mitandao ya kijamii @SelcomTanzania na @SelcomPesa na kwa namba za simu zinazopatikana bure ni 0800 784 888, 0800 714 888.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *