Na Mohammed Ulongo
Bahati Nasibu ya Taifa ya Tanzania, imetangaza rasmi ushirikiano na mtoa huduma wa malipo kwa njia ya simu nchini Selcom Tanzania, ili kuhakikisha Watanzania wanashiriki katika michezo ya bahati nasibu kwa urahisi mara tu Bahati Nasibu ya Taifa itakapozinduliwa rasmi.
Amesema ushirikiano huu utarahisisha upatikanaji, ununuzi na ulipaji wa tiketi kwa urahisi na usalama kote nchini kwa kutumia mifumo mbalimbali kupitia kampuni hiyo.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Mkurugenzi wa ITHUBA Tanzania, Bw. Kelvin Koka, wakati wa utiliaji saini na kampuni ya malipo nchini Selcom ambapo amsema Ushirikiano huwo na Selcom Tanzania ni hatua muhimu katika kuhakikisha kuwa Bahati Nasibu ya Taifa inawafikia Watanzania wote nchini. Kwa kutumia miundombinu madhubuti ya malipo ya Selcom.
Aidha, Koka amesema umuhimu wa ushirikiano huu na Selcom Tanzania ni hatua kubwa katika sekta ya michezo ya kubahatisha nchini, kwa kushirikiana na Selcom, tutahakikisha kuwa Bahati nasibu ya Taifa itakapozinduliwa kila Mtanzania bila kujali mahali alipo nchini, ataweza kushiriki kikamilifu katika michezo mbali mbali ya kusisimua ya bahati nasibu.
Kwa Upande wako Mkuu wa Kitengo cha masoko kutoka Selcom Bi. Shumbana Walwa amesema kushiriki katika michezo ya bahati nasibu kupitia USSD codes, mawakala wa selcom huduma ambao wapo zaidi ya 30000 nchi nzima,na vituo vya selcom 10 vilivyopo maeneo mbalimbali hapa nchini kutasaidia kuongeza washiriki wa bahati nasibu ya taifa nchi nzima.

Pia washiriki wa bahati nasibu ya taifa wataweza kununua tiketi na kupokea malipo ya ushindi kupitia majukwaa ya fedha kwa njia ya simu, USSD, hamisho kutoka benki, vituo vya malipo ya Selcom, na miamala ya kidijitali. Aidha, upatikanaji wa Selcom katika taasisi mbalimbali za kifedha utahakikisha kuwa hata wale wanaoishi maeneo yasiyofikika kiurahisi wanaweza kushiriki kikamilifu katika michezo ya bahati nasibu ya taifa.
Hata hivyo sehemu ya mapato yatokanayo na mauzo ya tiketi za bahati nasibu yatatengwa kwaajili ya miradi muhimu kama vile kuendeleza michezo ya vijana chipukizi, na sekta nyingine zinazo igusa jamii. Ushirikiano huu na Selcom utakuwa na mchango mkubwa katika kuongeza ushiriki.