Saudia yajibu kwa kauli kali matamshi ya kijuba ya Netanyahu kuhusu Palestina

Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudi Arabia imepongeza upinzani wa kimataifa dhidi ya matamshi ya kijuba ya waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu kuhusiana na Ukanda wa Ghaza na imepinga hatua yoyote ya kuhamishwa Wapalestina kutoka kwenye ardhi zao.