
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), limeufungulia Uwanja wa Benjamin Mkapa kutumika kwa mechi za kimataifa za kimashindano, uamuzi ambao umefanyika siku 15 baada ya shirikisho hilo kuufungia baada ya kubaini ubora duni wa eneo la kuchezea katika ukaguzi ambao lilifanya wiki mbili zilizopita.
Uamuzi huo unamaanisha kuwa Simba itautumia uwanja huo kwa mechi yake ya marudiano ya hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Al Masry ambao itakuwa nyumbani, Aprili 9 mwaka huu.
Taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo, Ijumaa, Machi 28, 2025 imeeleza kuwa CAF imeridhishwa na maboresho yaliyofanywa kwenye eneo la kuchezea la Uwanja wa huo.
“Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeuruhusu uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kutumika kwa michezo ya robo fainali na nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL) na Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC) 2024/2025.
“Uwanja huo umeruhusia baada ya Ukaguzi uliofanywa na Wakaguzi wa CAF hivi karibuni. CAF inaendelea kufuatilia kwa karibu maboresho yanayoendelea kwenye uwanja huo.
Mapema juzi, meneja habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally aliwatoa hofu mashabiki wa timu hiyo juu ya matumizi ya Uwanja wa Benjamin Mkapa ambapo alifichua kuwa CAF imewapa matumaini ya kuutumia.
“Niwatoe hofu kwamba Uwanja wa Benjamin Mkapa umeshafanyiwa ukaguzi. Bado majibu hayajatoka lakini katika mazungumzo wanasema kuna maboresho makubwa kwenye uwanja ukilinganisha na mara ya mwisho walipofanya ukaguzi.
“Hivyo kuna nafasi kubwa ya kucheza kwenye uwanja huo. Na wote mnakumbuka kauli ya Msemaji Mkuu wa Serikali alivyosema kwamba uwanja upo tayari. Hatuna muda wa kusubiri, sisi tunafanya maandalizi yote kuelekea Benjamin Mkapa kwa sababu tuna uhakikisho kutoka serik