Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo Machi 10, 2025 jijini Dodoma.
Kikao hicho kitafuatiwa na kile cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM (NEC). Hata hivyo, taarifa ya Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla haikuweka wazi ajenda za vikao hivyo, lakini imaaminika ni sehemu ya maandalizi ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

Tayari CCM imempitisha Rais Samia kuwa mgombea urais kwa Tanzania, Dk Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza huku Dk Hussein Mwinyi akipitishwa kwa Zanzibar.
Licha ya hatia hiyo, mchuano mkali umeanza kushika kasi kwenye majimbo ya ubunge na udiwani ambapo, makada wamekuwa wakipitapita kuanzisha harakati za kusaka uwakilisho huo.

Mara kadhaa viongozi wa juu wa CCM wamekuwa wakikemea wanaojipitisha na siasa chafu zinazoendelea kwenye majimbo na kutishia kuchukua hatua kwa mujibu wa kanuni zake.
Endelea kufuatilia Mwananchi.