
Kiongozi wa ngazi za juu wa harakati ya Hamas amesema: “Utawala ghasiibu wa Israel una dhana kwamba unaweza kufikia malengo yake, lakini Gaza iko na itasalia kuwa eneo la ardhi ya Palestina.”
Sami Abu Zuhri amesema katika mazungumzo yake na mtandao wa Al-Alam kwamba: Zimepita siku ya 415 za vita, na utawala ghasibu wa Israel unaendeleza vita vyake vya mauaji ya kimbari dhidi ya watu wetu katika Ukanda wa Gaza.
Ameongeza kuwa: Sambamba na vita vya mauaji ya wavamizi, bado tunashuhudia misimamo dhaifu ya baadhi ya nchi za Kiarabu na Kiislamu.
Abu Zuhri amesema: “Tunapongeza kwa fahari kuba mapambano ya watu wetu. Damu safi za taifa letu hazitapotea bure, bali zitakuwa mtaji wa mapambano yya kuikomboa nchi yetu.”
Afisa huyu mashuhuri wa Hamas ametangaza kuwa: Tunafanya kampeni kubwa zaidi na mashirika ya kimataifa na nchi rafiki ili kuharakisha utoaji wa misaada unaendelea huko Gaza.