Salva Kiir amteua makamu wa rais, hatua inayozua mijadala

Wakati Rais Salva Kiir ameanza kuwatimua baadhi ya wajumbe wa serikali yake na kuwateua viongozi wapya kuchukuwa nafasi ya waliotimuliwa, uteuzi wa Benjamin Bol Mel umeibua hisia nyingi. Lakini kwa uteuzi huu, Wasudani Kusini wengi wanaona kuwa Salva Kiir anaanda mrithi wake.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Juba, Florence Miettaux

Uteuzi huo ulifanyika siku moja baada ya kurejea kutoka Falme za Kiarabu, ambako alikaa wiki moja, ambapo Salva Kiir alitekeleza mabadiliko haya makubwa, “moja ya mabadiliko ya kisiasa ya kuvutia sana huko Juba” kulingana na mtafiti Daniel Akech Thiong wa Kundi la Kimataifa la utatuzi wa Migogoro (ICG). Katika msururu wa maagizo yaliyoibua gumzo la kisiasa, rais wa Sudan Kusini aliendelea kuwatimua baadhi ya wajumbe wa serikali na kuwateua viongozi wapya, akimfuta kazi mkuu wa idara ya ujasusi, mawaziri wawili, gavana wa eneo na makamu wawili wa rais.

Chaguo la la mrithi wa Salva Kiir?

Wakati huo huo, alitangaza uteuzi Benjamin Bol Mel kuwa makamu wa rais anayesimamia uchumi. Haya yote yanaonekana kuashiria chaguo la mrithi wa Salva Kiir, ambaye ana umri wa miaka 73. Kulingana na Daniel Akech Thiong, “baadhi ya vipengele vinaonyesha kuwa rais anawaondoa wapinzani wake watarajiwa ili kuandaa njia kwa mrithi wake, Benjamin Bol Mel.”

Mfanyabiashara huyo mwenye umri wa miaka 47 asiyependwa na wengi. Mshauri wa Rais Salva Kiir “kwa miradi maalum” tangu 2022, anashutumiwa na Washington kwa kupokea zaidi ya dola bilioni 3.5 katika kandarasi za umma za kujenga barabara ambazo hazijakamilika.

Athari kwenye kidiplomasia

Lakini kulingana na Daniel Akech Thiong, uteuzi wake unaweza kinyume chake “kuwaunganisha wapinzani wa Salva Kiir dhidi yake.”

Ingawa kuna malumbani ya ndani, uteuzi wa Benjamin Bol Mel kama makamu wa rais unaweza pia kuwa na athari ya kidiplomasia na Sudan, katika mazingira ambayo tayari yanatia wasiwasi. Kwa sababu uteuzi huo mpya kwa hakika una uhusiano fulani na Falme za Kiarabu, unaoshutumiwa kusaidia wanamgambo wa FSR katika vita dhidi ya jeshi la Sudani.