Salami: Tutalipa kisasi dhidi ya Israel na hilo halina shaka

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu la Iran SEPAH amesema kuwa, wananchi wa Iran lazima wawe na yakini kwamba tutalipiza kisasi kwa utawala ghasibu wa Israel.

Meja Jenerali Hossein Salami amesema hayo katika Manuva ya Kuelekea Baytul-Muqaddas yaliyojumuishwa mabasiji 60,000 katika mji wa Khustan kusini magharibi mwa Iran na kusisditiza azma ya Jamhuri ya kiislamu ya Iran ya kulipiza kisasi dhidi yya uchokozi wa majuma kadhaa wa Israel wa kukiuka mamlaka ya kujitawala taifa hili.

Kamanda Salami amesema, kuendelea kwa vita hivi kutapelekea tu kuangamizwa kwa Israel, na ikiwa Waislamu wataungana pamoja, chembechembe hii ya ufisadi itaangamizwa, na kwa hakika watu watapita katika njia hii, na ulimwengu hautadumu kwa ukatili.

Kamanda Mkuu wa jeshi la SEPAH amebainisha kuwa, tukiangalia kumbukumbu. ya waliotangulia tutaona kwamba maangamizi yanaingojea Israel; wananchi wa  wa Iran wanapaswa kuwa na uhakika kwamba tutalipiza kisasi kwa Israel.

Kadhalika Meja Jenerali Salami ameashiria kutolewa waranti wa kutiwa mbaroni Benjamin Netanyahu na aliyekuwa mshirika wake Yoav Gallant na kueleza kwamba, uamuzi huo ni ishara ya kufikia mwisho Israel ambayo imeendelea kutengwa kila leo  na kwamba, hukumu hiyo ni ushindi mkubwa kwa Umma wa Kiislamu.