Salami: Njama za US, Israel kudhuru Muqawama zimegonga mwamba

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC), Meja Jenerali Hossein Salami amesema, hakuna shaka kwamba juhudi za Marekani na utawala wa Kizayuni za kujaribu kuudhuru mrengo wa Muqawama zitafeli na kugonga mwamba.