Salami: IRGC ina ‘Akili Mnemba’ ya kutumia kwenye operesheni ngumu za kijeshi

Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) amesema kikosi cha wasomi cha jeshi hilo la Iran kimejizatiti kwa teknolojia ya Akili Mnemba ili kutekeleza vyema operesheni nzito na ngumu za kijeshi.