Dar es Salaam. Matukio katika picha kabla na wakati wa kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kinachoendelea muda huu makao makuu ya chama Mikocheni, jijini Dar es Salaam leo Jumatatu, Machi 10, 2025.

Kikao hicho kinaongozwa na Makamu Mwenyekitiwa chama hicho Zanzibar, Said Mzee Said. Anaongoza kikao hicho baada ya Mwenyekiti wa chama, Tundu Lissu, na Makamu Mwenyekiti -Bara, John Heche, asubuhi ya leo kwenda katika viwanja vya Karimjee, kumuaga Profesa Philemon Sarungi.


Lissu, Heche, na Mjumbe wa Kamati Kuu hiyo, Godbless Lema, wakitoa heshima za mwisho kwa Profesa Sarungi, watakwenda kuungana nao kwenye kikao hicho.

Endelea kufuatilia Mwananchi.