SADC na M23 watiliana saini makubaliano kuhusu kuondoka kwa SAMIDRC

Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na kundi la M23 linaloungwa mkono na Rwanda lililoiteka miji ya Goma na Bukavu miezi miwili iliyopita siku ya Ijumaa, Machi 28, walifikia makubaliano kuhusu utaratibu wa kuondolewa kwa kikosi kilichotumwa huko mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Wiki mbili zilizopita, SADC ilimaliza kazi ya SAMIRDC, ambayo imeshindwa kusitisha mashambulio ya hivi punde zaidi ya M23 mashariki mwa DRC ambako wanajeshi wake kadhaa waliuawa katika mapigano.

Wakuu wa majeshi wa Afrika Kusini, Jenrali Rudzani Maphwanya, mkuu wa majeshi ya Zambia, Jenerali Geoffrey Zyeele, wa Malawi, Meja Jenerali Saiford Kalisha na Meja Jenerali Ibrahim Michael Mhona wa Tanzania walikutana na mkuu wa jeshi la M23 Sultani Makenga katika mji wa Goma, kulingana na taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya mkutano huo.

Rais wa Zimbabwe wakati akizungumza katika mkutano wa awali wa viongozi wa SADC na EAC kuhusu hali ya DRC.
Rais wa Zimbabwe wakati akizungumza katika mkutano wa awali wa viongozi wa SADC na EAC kuhusu hali ya DRC. © Ikulu ya Tanzania

Kwa Pamoja wamekubaliana kuufungua upya uwanja wa ndege wa kimataifa wa ndege, baada ya kuukarabati upya, ili kuruhusu vikosi vya SADC kuondoka, kukabidhiwa kwa waasi wa M23, silaha zote zilizohifadhiwa na SADC ambazo zilikuwa zikitumiwa na jeshi la Congo FARDC na pia kuruhusu vikosi vya SAMIDRC kuzunguka kwa uhuru katika maeneo ya Goma.

Pia maafisa hao wamekubaliana kukutana tena katika siku za hivi karibuni, katika kutathmini hali halisi ya mambo kabla ya kuanza kutekeleza makuabaliano yote hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *