Sadaka ina nguvu kukupatanisha na Mungu, kufungua vifungo

Bwana Yesu asifiwe, kwa neema ya Mungu tena nimepata kibali kukuletea somo lihusulo sadaka.

Wakristo wengi hatujui kutoa sadaka, hata kama tunatoa tumetumia muda mwingi kulaumu kwa nini huyu mtumishi anakula sadaka yangu, lakini pia tunatoa sadaka na kuangalia fedha tutoayo pasipo kujua kuwa tunamtolea nani?

Ukweli ni kwamba sadaka ya namna yoyote unayotoa lazima uwe na ufahamu kuwa unatoa kwa Mungu hata kama wewe unaona mtumishi ndiyo yupo mbele yako, lakini wewe jiunganishe na Mungu aliye hai kwa kuiambia sadaka ifanye kitu fulani kwenye maisha yako na Mungu hataangalia ni kiasi gani umetoa, yeye ataangalia ni maneno gani yameambatana na sadaka yako. Hivyo lazima ujiunganishe na Mungu katika utoaji wako.

Katika Mwanzo 1-14 ukisoma mistari yote utakutana na kisa hiki kwa undani… Ibrahimu akajenga madhabahu huko, akaziweka tayari kuni, kisha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile kuni. Ibrahimu akanyoosha mkono wake, akakitwaa kisu ili amchinje mwanawe. Ndipo malaika wa Bwana akamwita kutoka mbinguni, akasema, Ibrahimu! Ibrahimu! Naye akasema, Mimi hapa. Akasema, Usimnyoshee kijana mkono wako, wala usimtendee neno; kwa maana sasa ninajua ya kuwa unamcha Mungu…

Tunachojifunza sadaka hutuunganisha mioyo yetu na Mungu wetu wa mbinguni aliyehai na kujua uaminifu wetu juu kuhusu kumtolea kwa moyo wa kupenda.

Vilevile, Mwanzo 14:17 Abramu aliporudi baada ya kumshinda mfalme Kedorlaoma na wale wafalme waliojiunga naye, mfalme wa Sodoma akatoka kwenda kumlaki katika bonde la Shawe (yaani, Bonde la Mfalme.) 18 Ndipo Melkizedeki mfalme wa Salemu alipoleta mkate na divai. Alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana. 19

akambariki Abramu, akisema, “Abarikiwe Abramu na Mungu Aliye juu sana, Muumba wa mbingu na nchi. 20 Abarikiwe Mungu aliye juu sana, ambaye amewaweka adui zako mkononi mwako.’’

Sadaka ni nini?

Sadaka ni shukrani na maombi yetu kwa Mungu wetu, na sadaka inatolewa kwa ajili ya kushukuru jambo fulani au inatolewa kuomba kutendewa jambo fulani, kama shukrani kwa ajili ya kujiunganisha na Mungu katika yale uliyotendewa au katika yale unayotamani kutendewa.

Sadaka inakuunganisha na Mungu na kuwa na hisa katika hazina za mbinguni, ndiyo maana yule anayetoa anajua anamtolea nani, sadaka ile inafanyika kuwa baraka kuliko kitu chochote kile.

Kwa nini tunapaswa kutoa sadaka?

Sadaka ni mali ya Mungu:- Walawi 27:30 ‘Zaka ya kila kitu kutoka shambani, ikiwa ni nafaka kutoka kwenye ardhi, au tunda kwenye miti, ni mali ya Bwana, ni takatifu kwa Bwana.

Sadaka ni ukombozi na upatanisho:- Walawi 16:20 “Aroni atakapokuwa amemaliza kufanya upatanisho kwa ajili ya patakatifu pa patakatifu, hema la kukutania na madhabahu, atamleta mbele yule mbuzi aliye hai. 21 Ataweka mikono yake miwili juu ya kichwa cha mbuzi aliye hai na kuungama juu yake uovu wote na uasi wa Waisraeli pamoja na dhambi zao zote, kisha kuziweka juu ya kichwa cha huyo mbuzi.

Tunajifunza kuwa sadaka ni ukombozi na upatanisho katika maisha, tunamuona Aroni anafanya upatanisho kwa ajili ya patakatifu kwa kuungama juu yake uovu wote na uasi wa Waisraeli pamoja na dhambi zao zote, kisha kuziweka juu ya kichwa cha huyo mbuzi, maana yake hapa sadaka ambaye ni mbuzi aliwekwa mbele ya kuhani ili iwe ukombozi na upatanisho na dhambi zao zote, kwani mbuzi huyo alibeba dhambi zote za Aroni na wana wa Israel wote.

Kupitia sadaka hiyo Mungu aliondoa maovu yote na shida zote na hatimaye Mungu alionekana kufanya sawasawa na maneno yao.

Katika maisha tunayoishi sasa tunasikia na kuona namna waganga na wachawi wakiwaambia watu wapeleke vitu wanavyopenda kama ni fedha, mali na wengi, hudiriki kuwapa masharti ya kutoa wapendwa wao, mwishowe wakiwaelekeza waombe wanayotaka wafanyiwe kupitia kile walichokitoa, hivyo miungu inafanya kile walichokiomba.

 Wewe Mkristo Mwamini Mungu pekee aliyehai na aliyechanzo cha uzima wetu, hupaswi kuangukia kwa waganga kwa sababu amesema yeye mwenyewe kwamba ametolewa sadaka pale msalabani ili sote tupate kupona. Kumbe sadaka wakati mwingine hutuponya na maovu yetu na kututakasa kabisa.

Huna sababu ya kuhangaika kwa waganga wala kutafuta nguvu za kukusaidia, bali kaa miguuni kwa Mungu na mtolee sadaka ujiunganishe na Muumba wetu.

Ni maombi yangu leo, usimame na kubadili njia mbaya kwa Jina la Yesu Kristo aliyehai. Mtolee Mungu wetu sadaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *