
Kwa mujibu wa taratibu za Kanisa Katoliki mazishi ya Papa hufanyika siku ya 4 hadi 6 baada ya kifo chake.
Sehemu kubwa ya maziko ya papa huwa anayapanga mwenyewe na kumwachia Kardinali Carmelengo jukumu la kutekeleza.
Baada ya kufa mwili hukabidhiwa familia ya Signoracci kwa ajili ya kuandaa mwili kwa ajili ya maziko. Mwili wa Papa labda aseme vinginevyo huzikwa ndani ya majeneza matatu, mbao nyepesi, fedha na mbao ngumu yanaowekwa moja ndani ya jingine.
Kwa kawaida mapapa huzikwa katika Basilika la Mtakatifu Peter ambapo tayari mapapa 91 wamezikwa.
Papa wa mwisho kuzikwa nje ya Vatican ni leo wa 13 ambaye alifariki mwaka 1903 ambaye alizikwa Basilika la Mtakatifu John Lateran.
Hata hivyo, Baba Mtakatifu amebadili kanuni hizi na kwa sasa Baba Mtakatifu ataziwa kwenye majeneza mawili tu, jeneza la mbao na jeneza la fedha.
Kitamaduni, jeneza la kwanza linatengenezwa na mti wa mvinje (cypress -mbao nyepesi) hili likiashiria unyenyekevu na ya kuwa Baba Mtakatifu alikuwa binadamu kama wengine jeneza hili pia litawekwa nakala ya ibada ya maziko; kibegi kidogo chenye sarafu za silver, shaba na dhahabu zinazotengenezwa kwa kila mwaka wa upapa wake, pallium na maandishi yanayoelezea kazi za baba mtakatifu aliyefariki.
Jeneza la pili ni la lead (risasi) ambayo ni madini ya hali ya chini (very humble metal) likiashiria usafi wa ndani, kinyume na chuma yanayong’aa na kumeremeta likiwa na maandishi anayenichagua mimi lazima aache yote aliyonavyo.
Katika jeneza hili za madini ya risasi ndani yake huwekwa maandiko yaliyotolewa na baba mtakatifu husika. Nje ya jeneza hili waliweka idadi ya miaka Papa mhusika aliyohudumu.
Jeneza la tatu linatengenwa na mbao ngumu ya mti wa mwaloni (Oak), ambalo linaashiria ukuu (dignity).
Mti huu unazungumzia ndani ya kitabu cha Hosea 4:13 kama mwaloni … ni mti mashuhuri kuko huko katika nchi ya Palestina mara nyingi unatumika kuweka mipaka au kuonesha maeneo maana unaishi muda mrefu. Ndani ya jeneza hili kuna chombo cha shaba ambapo ndani yake wanaweka mafanikio ya baba mtakatifu husika.
Kila jeneza linapofungwa, linazungushiwa vipande viwili vya kamba ya hariri na pia kuwekewa mhuri wa Kardinali Carmelengo na ule wa Kardinali Amidi.
Wakati wa ibada na kutoa heshima za mwisho mwili wa baba mtakatifu aliyefariki huwekwa kwenye ubao tu na huwa wazi kuanzia kichwani hadi kwenye miguu akiwa amevalia mavazi kamili ya kipapa.
Ni wakati wa maziko tu ndipo mwili huu unawekwa kwenye majeneza matatu (au mawili kama ambavyo Papa Fransis amebadili mabadiliko). Baada ya ibada na kuaga mwili wa Baba Mtakatifu unazikwa katika makaburi yaliyo chini ya Kanisa la Mtakatifu Petro au kama ambavyo Baba Mtakafitu atakavyokuwa ameelekeza.
Papa Fransis yeye atazikwa katika Basilika la Santa Maria Maggiore, lilipo Roma.
Hii imeenda kinyume na tamaduni za muda mrefu ambapo mababa watakatifu huziwa katika mapango yaliyo chini ya kanisa la Mt. Petro Roma.
Amechagua eneo hilo kwa sababu ndipo anapotembelea mara nyingi anapokuwa na ziara za kimataifa.
Hata hivyo, Vatican imefanyia marekebisho makubwa namna ya kumzika Papa katika waraka wa Ordo Exsequiarium Romani Pontificis, uliorekebishwa kwanza na Papa Yohani Paul II na kurekebishwa zaidi na Papa Fransis na kusainiwa Aprili 2024 na kutolewa kwa umma Novemba 19, 2024 na ofisi ya kipapa inayohusika na liturgia za kipapa.
Idadi ya majeneza imepunguzwa kutoka matatu hadi mawili, na mwili wa Papa aliyefariki utaangaliwa
kwenye jeneza na si kwenye ubao wa wazi kama ilivyokuwa awali.
Sheria hizi zimesainiwa na Baba Mtakatifu Fransisko Aprili 2024 ambazo kimsingi zilipitishwa awali na Papa Jouhn Paul II na kutangazwa mwaka 2000.
Mabadiliko hayo yalitafsiriwa na wengi kuwa yanalenga kuonyesha kuwa maziko ya Papa ni ya mchungaji na mfuasi wa Kristo na si ya mtu maarufu sana duniani.
Kwa waraka huu wa sasa, Ordo Exsequiarium Romani Pontificis, maziko ya Papa yatafuata hatua tatu muhimu. Kwanza ni misa ndani ya kanisa la kipapa na Papa atakuwa katika jeneza la wazi.
Kisha hapo mwili wa Papa utaweka katika jeneza la mti wa mvinje na kufunikwa na ibada ya maziko kufanyika katika viwanja vya Mtakatifu Petro na sehemu ya tatu, ni ibada ya kuuweka mwili kaburini sehemu atakayokuwa amechagua Papa kabla ya kufariki.
Kwa taratibu za awali jeneza la mvinje litafungwa na utepe mwekundu na kuweka mhuri, kisha linawekwa kwenye jeneza la madini ya zebaki na mwishoni linawekwa kwenye jeneza la mbao ngumu na kufungwa kwa misumari ya dhahabu.
Ndani ya jeneza la mvinje wataweka nyaraka inayoonyesha mafanikio ya Papa; ndani ya jeneza la zebaki wataweka mifuko midogo yenye sarafu za shaba, fedha na dhahabu kwa idadi ya miaka ya upapa wake, kila mwaka sarafu moja moja.
Mabadiliko mengine ni namna ya kuthibitisha kifo cha Papa. Mwanzoni zoezi hili lilifanyika katika chumba ambacho Papa amefariki, ila kwa mabadiliko haya ya Ordo Exsequiarium Romani Pontificis, sasa uthibitisho utafanyika katika Kanisa binafsi la Papa. Badiliko jingine ni namna ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Papa, ambapo kwa sasa hautawekwa tena kwenye ubao wa wazi (Canaletto) au kitanda cha kifo kwa Kilatini, badala yake utaweka kwenye jeneza la wazi la mbao lenye mstari wa zebaki na utapelekwa moja moja katika Kanisa la Mtakatifu Petro, bila kupitia katika makazi ya Papa kwa ajili ya watu kutoa heshima za mwisho.
Wakati wa suala hili la kuupeleka mwili kwenye kanisa la Mtakatifu Petro, wimbo wa litania za watakatifu utakuwa unaimbwa baada ya kuboreshwa na kuongezea watakatifu wa siku za karibuni.
Badiliko la mwisho kubwa ni hilo la wapi mwili utazikwa, waraka unabainisha kuwa Papa anaweza kuzikwa nje ya viunga vya Vatikani.
Baada ya sehemu ya tatu, yaani maziko ya baba katika eneo atakalokuwa amechagua, itafuatwa na kitu kinaitwa novemdiales, yaani siku tisa za misa takatifu, kila siku kardinali mmoja akiteuliwa kuongoza misa.
Baada ya hapo imekuwa ni utamaduni kwa Papa aliyefariki kusomewa misa 100 kwa ajili ya kuomboleza na kumwombea. Hii ni kwa sababu, wajibu unavyokuwa mkubwa, uwezekano wa kufanya makosa na dhambi ni mkubwa zaidi na hivyo maombi zaidi yanahitajika.
Kwa miaka ya 1585 hadi mwaka 1903, kulikuwepo utamaduni wa kuzika tofauti moyo na mapafu ya Papa aliyefariki katika kanisa dogo la Sancti Vincenso e Anastasio, kwenye chemichemi ya Trevi.
Eneo hili ni parokia karibu na jumba la kipapa la Quirinal, ambapo maPapa walikuwa wanaishi.
Hii ilitokana na imani kuwa Wakatoliki inabidi wazikwe kwenye parokia walizotoka na kwa kuwa mapapa walikuwa wanaishi katika eneo hilo, angalao sehemu ya mwili wao ilizikwa katika kanisa hili kudhihirisha hilo.
Nyongeza na Stephen Luke Kirama ambaye ni Mwanafunzi wa TaaliMungu na Historia ya Katoliki