Rwanda yasikitishwa na madai ya rais wa Burundi kuhusu njama ya uvamizi

Rwanda imesema imesikisitishwa na madai, ambayo inasema ni ya kusikitisha yaliyotolewa na rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye, kuwa Kigali inapanga kuishamnbulia.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Kauli hii ya Rwanda, imekuja baada ya rais Ndayishimiye, kuliambia Shirika la Habari la Uingereza BBC kuwa, alikuwa amepokea ripoti za kuaminika za Kiiteljensia, nchi hiyo jirani ilikuwa inapanga kuishambulia.

Aidha, kiongozi huyo wa Burundi, ameishtumu Rwanda, kwa kuwa nyuma ya jaribio la mapinduzi ya mwaka 2015, kitendo alichodai kuwa ndicho kinachoendelea kwa sasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Hata hivyo, Olivier Nduhungirehe Waziri wa Mambo ya nje wa Rwanda, akimjibu rais Ndayishimiye, amesema kauli ya kiongozi huyo inasitisha na kuongeza kuwa Rwanda inahusika kwenye mchakato wa upatikanaji wa suluhu Mashariki mwa DRC.

Aidha, amesema kuwa wanajeshi wa Rwanda na Burundi na maafisa wa Inteljensia, wanahusika kwenye mazungumzo ya kiiteljensia kuhusu kuhusu namna ya kutatua mzozo wa DRC.

Hii sio mara ya kwanza, kwa Burundi ambayo ilifunga mpaka wake Rwanda mwaka uliopita, imekuwa ikiishtumu nchi hiyo jirani kwa kuwaunga mkono waasi wa RED TABARA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *