Rwanda yadhibiti idadi ya wanaohudhuria mazishi baada ya mlipuko wa virusi vya Marburg

Serikali ya Rwanda imetangaza kuwa, inatekeleza mpango wa kudhibiti idadi ya watu wanaohudhuria mazishi ya waathiriwa wa virusi vya Marburg katika juhudi za kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa huo unaoambukiza kwa kasi.