Rwanda yaadhimisha kumbukumbu ya miaka 31 ya mauaji ya kimbari

Rwanda inaadhimisha miaka kumbukumbu ya miaka 31 ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 yaliyopelekea mauaji ya watu 800,000 katika muda wa siku 100.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2

Matangazo ya kibiashara

Siku 100 za huzuni ambapo kiza bado kinatanda katika nchi hii ya Maziwa Makuu ya Afrika, licha ya kazi ya maridhiano isiyo na mwisho.

Sherehe rasmi zinaanza Aprili 7 – siku ya mauaji ya kwanza ya kile kilichokuwa mauaji ya mwisho ya halaiki katika karne ya 20, na kusababisha vifo vya watu 800,000, haswa miongoni mwa Watutsi walio wachache, lakini pia Wahutu wenye msimamo wa wastani.

Kama kila mwaka, Rais Paul Kagame – kiongozi wa Rwandan Patriotic Front (RPF) ambaye alipindua utawala wa Kihutu wa mauaji ya halaiki mnamo mwezi Julai 1994 na amekuwa shujaa wa nchi hiyo tangu wakati huo – atawasha mwali wa ukumbusho kwenye Kumbukumbu ya Gisozi mjini Kigali.

“Mende”

Mauaji ya majira ya kuchipua 1994 yalichochewa siku moja baada ya shambulio la ndege ya rais wa Kihutu Juvénal Habyarimana, katika hali ya chuki iliyochochewa na propaganda mbaya dhidi ya Watutsi.

Kwa muda wa miezi mitatu, jeshi, wanamgambo wa Interahamwe na pia raia wa kawaida waliwaua kwa bunduki, mapanga au marungu – Watutsi, walioitwa “Inyenzi” (“mende” kwa lugha ya Kinyarwanda), lakini pia wapinzani wa Kihutu. Mauaji hayo yaliisha wakati waasi wa Watutsi wa RPF walipoteka Kigali mnamo Julai 4, na kusababisha mamia ya maelfu ya Wahutu walio kuwa na hofu kuhama kwenda Zaire (sasa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo).

Miaka 30 baadaye, makaburi ya halaiki yanaendelea kufukuliwa. Jumuiya ya kimataifa ilikosolewa vikali kwa kutochukua hatua, na Umoja wa Mataifa kwa kuondoa vikosi vyake baada ya ghasia za kwanza.

“Nguvu tofauti”

Kwa miaka 30, Rwanda imekuwa ikifanya kazi ya upatanisho, hasa kwa kuundwa mwaka 2002 kwa mahakama za kijamii, “gacaca” ambapo waathiriwa wanaweza kusikiliza “maungamo” ya wauaji.

Kadi za utambulisho hazitaji tena ukabila, na historia ya mauaji ya halaiki inafunzwa katika mtaala unaodhibitiwa vilivyo. Leo, zaidi ya 70% ya watu milioni 13 wa Rwanda wana umri wa miaka 30 au chini. Bila kusahau yaliyopita, wanakusudia kujikomboa kutoka katika uzito wa mauaji ya kimbari ambayo hawakushuhudia.

Vyombo vya sheria pia vilichukua jukumu kubwa lakini kulingana na Kigali, mamia ya watu wanaoshukiwa kushiriki katika mauaji ya halaiki bado wako huru, haswa katika nchi jirani, kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na Uganda.

Mivutano ya kidiplomasia

Hata hivyo, uhusiano haujatulia na DRC ambayo, kulingana na ofisi ya mwendesha mashtaka wa Rwanda, inahifadhi idadi kubwa ya washukiwa waliokimbia (408). Shutuma za pande zote za uvunjifu wa amani zimekuwa za mara kwa mara tangu kumalizika kwa mauaji ya kimbari. RPF ilishutumiwa kwa kuua makumi ya maelfu ya watu nchini Zaire (DRC sasa) katika kuwasaka wahusika wa mauaji ya halaiki.

Mvutano umeongezeka kwa kasi tangu mashambulizi ya M23, waasi wengi wao kutoka jamii ya Watutsi, mwishoni mwa mwaka 2021 mashariki mwa DRC. Kinshasa, pamoja na Umoja wa Mataifa, Marekani na nchi kadhaa za Magharibi zinaishutumu Kigali kwa kuwaunga mkono waasi hao. Kigali inakanusha kuhusika na inashutumu DRC kwa kuunga mkono kundi la Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR), kundi lenye Wahutu wengi lililoundwa na maafisa wakuu wa zamani wa mauaji ya halaiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *