Rwanda: Uchunguzi dhidi ya Agathe Habyarimana umemalizika bila kufunguliwa mashtaka

Uchunguzi nchini Ufaransa dhidi ya Agathe Habyarimana – mjane wa rais wa zamani wa Rwanda Juvénal Habyarimana – sasa umefungwa bila kufunguliwa mashtaka yoyote. Uamuzi uliofanywa siku ya Ijumaa, Mei 16, 2025, kulingana na vyanzo vilivyo karibu na kesi hiyo. Majaji walihitimisha kuwa ushahidi unaomtia hatiani kwa jukumu lake katika mauaji ya halaiki ya mwaka 1994 “unapingana, hauendani na ni uongo mtupu.”

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika agizo lililoandikwa siku ya Ijumaa, majaji wanaosimamia kesi hiyo walihitimisha kuwa “katika hatua hii hakuna ushahidi wa dhati na thabiti dhidi ya Agathe Habyarimana kwamba aliweza kushiriki katika mauaji ya kimbari […]. Ikiwa uvumi huo utaendelea, majaji wanaongeza, hauwezi kuwa uthibitisho kwa kukosekana kwa vipengele vya kina na vinavyolingana.”

Kulingana na majaji hao, hakuna hotuba ya umma ya Agathe Habyarimana inayotoa matamshi ya chuki au kutaka mauaji ya halaiki.

Uchunguzi sasa umefungwa – bila mjane wa rais wa zamani kushtakiwa. Agathe Habyarimana amekuwa mlengwa wa uchunguzi nchini Ufaransa tangu mwaka 2008 kwa kuhusika katika mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu. Uchunguzi ulifunguliwa kufuatia malalamiko kutoka kwa Muungano wa Vyama vya Kiraia vya Rwanda.

Akiwa na umri wa miaka 82, hadi sasa hakabiliwi na kesi yoyote. Uamuzi huu unakuja wakati ofisi ya mwendesha mashtaka wa kitaifa wa kupambana na ugaidi, ambayo ina mamlaka katika suala hili, ilipeleka suala hilo kwenye chumba cha uchunguzi cha Mahakama ya Rufaa ya Paris mnamo mwezi Septemba 2024 kwa nia ya kumfungulia mashtaka. Kesi pia imepangwa kufanyika siku ya Jumatano, Mei 21.

Ofisi ya mwendesha mashtaka wa Paris na wanaoiendesha wana wasiwasi kwamba kesi hiyo inaweza kuamriwa kumpendelea Bibi Habyariamana; kwa sababu anafikiria – na tunaweza kufikiria pamoja naye – madhara ambayo yanaweza kuwa kwa upande wa Kigali, amesema Wakili Philippe Meilhac, mwanasheria wa Agathe Habyarimana.

Mwanasheria wa Shirikisho la Kimataifa la Haki za Kibinadamu (FIDH) – chama cha kiraia – alichukizwa na ukosefu wa mashtaka, ingawa, kulingana na yeye, kuna “ushahidi wa kutosha” dhidi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *