Rwanda na DR Congo zawekaa makataa ya Mei 2 kwa makubaliano ya amani

Rwanda na jirani yake DRC zimekubaliana kufanyia kazi rasimu ya makubaliano ya amani ifikapo Mei 2 kufuatia miezi kadhaa ya ghasia zinazoendelea mashariki mwa DRC.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Siku  ya Ijumaa nchi hizo jirani ziliafikia kufanyika  kazi rasimu ya makubaliano ya amani ifikapo Mei 2 na kuapa kuheshimu uhuru wa kila nchi, hatua inayokuja baada ya waasi kuripotiwa kupiga hatua kubwa mashariki ya DRC.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Rwanda, ambayo imekuwa ikikabiliwa na ukosoaji kwa kuwaunga mkono waasi wa M23, na mwenzake wa DR Congo, ambayo imeshuhudia miji yake mikubwa ikitekwa na waasi mashariki yake DRC walitia saini rasimu ya makubaliano mjini Washington mbele ya Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio.

Kulingana na rasimu hiyo, nchi hizo mbili zinatambua uhuru wa kila mmoja na uadilifu wa eneo na kujitolea katika njia ya kutatua mizozo yao kwa njia za amani kwa njia ya  diplomasia na mazungumzo badala ya kutumia nguvu za uhasama au matamshi.

Bila kuwataja waasi wa M23 kwa uwazi, taarifa hiyo ilisema kuwa nchi zote mbili zilikubali malalamiko ya  nchi nyingine na zitajizuia kutoa msaada wa kijeshi na wa serikali kwa makundi yasio ya serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *