
M23 inayoungwa mkono na Rwanda yuko rasmi katika mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kusini, Bukavu, tangu mapema Jumapili asubuhi. Msemaji wa jeshi la Kongo amethibitisha uwepo wa waasi hao katika mji wa Bukavu. Zaidi ya hayo, takriban kilomita arobaini kuelekea kusini, kwenye mpaka kati ya Bugarama nchini Rwanda na Kamanyola nchini DRC, vivuko kwenye kituo cha mpaka vilifungwa sku ya Jumapili kutokana na kutokuwa na uhakika na hali ya usalama.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Chini ya kivuli cha lori lake, akiwa amekaa na madereva wengine, Nicolas Muhemedi anasubiri kwa siku mbili ili aweze kuvuka mpaka kurejea Uvira: “Tupo hapa, tumekwama, hatujui kinachoendelea. Tulifika hapa jana (Jumamosi) asubuhi, tukasikia milio ya risasi, hivyo polisi wakatuambia tuondoe magari yaliyokuwa hapa twende upande wa pili. “
Katika kituo cha mpakani, maafisa wa uhamiaji wa Kongo walionekana mara ya mwisho siku ya Ijumaa, Februari 14. Milio mingi ya risasi ilisikika hadi Bugarama nchini Rwanda katika siku za hivi karibuni, wanasema wakazi wengi kama Amose Ngamije: “Hakuna aliyevuka leo [Jumapili] au jana [Jumamosi]. Kulikuwa na wahalifu waliotaka kuiba na kupora, walipiga risasi nyingi nchini mwao, lakini hapa Bugarama hakukuwa na shida. “
Siku ya Jumapili hali ya utulivu ilirejea ambapo shughuli zilianza tena katika mji wa Bugarama nchini Rwanda. Akiwa na mtoto wake mikononi mwake, Tarcila Nyirashyirambere anatoka tena barabarani, baada ya kurejea hali ya utulivu. “Hapa Bugarama mambo ni mazuri leo, lakini Jumamosi tulikuwa na wasiwasi, tulisalia majumani kwetu hakuna aliyetoka, wengine walifikiria kukimbia, lakini risasi zilikatika mchana na tukaamua kubaki. “
Kutoka Mto Rusizi, unaotenganisha Rwanda na uwanda wa Kamanyola nchini DRC, hakuna mtu aliyeonekana kwenye kingo za Kongo siku ya Jumapili. Idadi ndogo ya watu ilionkana baadhi wakifanya shughuli zao kuelekea kusini, huku wengi wakikimbilia nchini Burundi.