
Maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 31 ya mauaji ya halaiki yaliyotekelezwa dhidi ya Watutsi na Wahutu wenye msimamo wa wastani nchini Rwanda mwaka 1994 yameanza Jumatatu, Aprili 7. Lakini mwaka huu, Rais Paul Kagame pia ametumia hotuba yake kwenye Ukumbusho wa Kitaifa wa Gisozi kukemea ukosoaji na shutuma zilizolenga nchi yake katika mzozo unaosambaratisha eneo jirani la Mashariki mwa DRC.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Kigali, Lucie Mouillaud
Siku za nyuma zilizokumbwa na giza na sasa za ukatili: kwa Rais wa Rwanda Paul Kagame, mambo yote hayo mawili hayawezi kutenganishwa, na Wanyarwanda lazima wachague kati ya kupigana au kuruhusu hali maya kuwakumba. Rwanda haiwezi kukubali hatua za kuiadhibu, anasema.
“Iwapo mtu yeyote atajitokeza na kusema anataka kutuadhibu, atakiwa aingizwe jahanama. Aingizwe tu kirahisi jahanama. Je, una matatizo yako mwenyewe ya kukabiliana nayo? Nenda ukayashughulikie na mimi nishughulikie yangu. “Ni katika mtazamo huu, nadhani, Wanyarwanda wanapaswa kuyachukulia maisha yao ya kila siku,” amesema.
Katika mzozo unaosambaratisha mashariki mwa DRC, simulizi inataka kuwaonyesha wahasiriwa kama wuaji, anasisitiza mkuu wa nchi, ambaye anakataa shutuma dhidi ya Rwanda na kukemea matamshi ya chuki na unyanyapaa wa Watutsi wa Kongo.
Katika Kumbukumbu ya Kitaifa ya Gisozi, Paul Kagame aliwasha mwali wa ukumbusho asubuhi ya Jumatatu, Aprili 7, kuashiria uzinduzi wa shughuli za ukumbusho kwa kipindi cha kila mwaka cha siku 100 kuenzi kumbukumbu ya wahasiriwa wa mauaji ya kimbari.
Baada ya sherehe rasmi, zaidi ya vijana 2,000 walianza maandamano ya ukumbusho mjini Kigali, ikiwa ni wakati wa ishara kwa Nathanael Mugisha: “Ili kusonga mbele, ni lazima tujue ni nini kilitokea, kuelewa nchi inatoka wapi na inaelekea wapi. Kwa hiyo ni muhimu, kama vijana, kuwepo, kujifunza historia ya nchi yetu na kuijua zaidi.”
Maandamano hayo yalifuatiwa na mkesha wa usiku katika uwanja wa BK Arena, ukimulikwa kwa mishumaa iliyobebwa na washiriki wote, kwa ajili ya kuwaenzi waliotoweka katika mauaji hayo ya kimbari.