Rwanda: London haitatuma malipo zaidi baada ya makubaliano ya wahamiaji kufutwa

Serikali ya Uingereza imesema haitatuma malipo zaidi kwa Rwanda kufuatia kufutwa kwa makubaliano ya mkataba wa wahamiaji kati ya nchi hizo mbili.

Imechapishwa:

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa serikali ya Rwanda, Yolande Makolo, alisema Uingereza iliitaka Rwanda “kuacha kudai” malipo yaliyosalia – yanayoripotiwa kufikia dola za Marekani milioni 64.

Mzozo wa malipo unaohusishwa na mpango wa Rwanda unakuja baada ya serikali ya Uingereza kutangaza kuwa itasitisha msaada kwa nchi hiyo, isipokuwa “msaada kwa watu maskini na walio hatarini zaidi”.

Uingereza ilichukua uamuzi wa kusitisha misaada baada ya kuishutumu Kigali kwa kuunga mkono kundi la waasi la M23 ambalo limeteka maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Mpango wa kuwafukuza baadhi ya waomba hifadhi nchini Rwanda, uliobuniwa na serikali ya chama cha Conservative mwaka 2022, uligharimu Uingereza dola milioni 310 kabla ya kuondolewa na Waziri Mkuu Sir Keir Starmer.