Rwanda: Kigali yafanya mazungumzo na Washington kuwapokea wahamiaji kutoka Marekani

Baada ya makubaliano ya uhamiaji kutelekezwa mwaka jana na London, je, Rwanda inaweza kutia saini mkataba mpya, wakati huu na Washington?

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu nchini Rwanda, Lucie Mouillaud

Majadiliano yanaendelea, Kigali inasema, wakati utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump unatafuta kuharakisha kuwafukuza wahamiaji kutoka Marekani. Katika televisheni ya taifa, Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda Olivier Nduhungirehe amethibitisha kwa mara ya kwanza kwamba majadiliano baina ya nchi hizo mbili na Marekani yanaendelea kuhusu makubaliano yanayowezekana kuhusu wahamiaji. Majadiliano yanaendelea, bado yako katika hatua ya “awali”, amesema, bila kutoa maelezo zaidi juu ya yaliyomo kwenye majadiliano.

Uwazi kwa masuala ya uhamiaji

Mkataba kama huo sio mpya kwa Rwanda, ameongeza mkuu huyo wa diplomasia, akimaanisha hasa mradi wenye utata uliotiwa saini mwaka 2022 na Uingereza, hatimaye kutelekezwa kabla ya kutekelezwa mwaka jana na serikali mpya ya Uingereza. Mamlaka ya Kigali – wakati huo – imethibitisha kwamba wanabaki kujitolea kwa masuala ya uhamiaji na wako wazi kwa majadiliano sawa na nchi nyingine.

Mwanzoni mwa mwezi Aprili 2025, Rwanda tayari ilitajwa na vyombo vya habari vya Marekani kama mojawapo ya nchi za tatu zilizofikiriwa na Washington kutuma wahamiaji waliokataliwa na utawala wa Marekani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *