
Rais wa Rwanda Paul Kagame amefanya mkutano wake wa kwanza mjini Kigali siku ya , Machi 16, mbele ya maelfu ya watu tangu kuchaguliwa tena Julai mwaka jana. Mkutano wenye mada kuu: mzozo wa mashariki mwa DRC. Hii ilikuwa ni fursa kwa mkuu wa nchi ya Rwanda kushutumu vikwazo vya kimataifa dhidi ya Rwanda na jukumu lililotekelezwa na baadhi ya nchi hususan Ubelgiji katika utekelezaji wa vikwazo hivyo.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwanahabari wetu mjini Kigali, Lucie Mouillaud
Mbele ya maelfu ya watazamaji, Rais wa Rwanda Paul Kagame almetetea juhudi za kikanda za SADC na EAC kutafuta suluhu la mzozo wa mashariki mwa DRC. “Jana [EAC] walikutana Nairobi, na sasa [EAC/SADC] watakutana Harare. “Huu ni mwanzo wa kuelekea kwenye suluhu ya kisiasa ya tatizo hilo, lakini itakuwa ni safari ndefu, kwani linapokuja suala la siasa kila mtu ana masilahi yake,” amesema.
Paul Kagame pia amerelea katika maendeleo ya mazungumzo ya kikanda kwa ajili ya njia ya kuondokana na mgogoro huo.
Rais Paul Kagame amelaani vikali vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Rwanda na nchi kadhaa. Vikwazo pia vilishutumiwa na washiriki, kama vile Jean Niyiteka: “Kuna mchakato wa kidiplomasia ambao matatizo haya yanaweza kutatuliwa. Hatutaki vikwazo hivi kwa nchi yetu, tunataka kuwa na uwezo wa kuendelea katika njia ya maendeleo.”
Katika hotuba yake kali, rais amelaani jukumu la Ubelgiji, inayochukuliwa kuwa mwanzilishi wa hatua za adhabu dhidi ya Kigali. Kwa wengi, Fredrick Sibomana anasema katika safu, msimamo wa Rwanda katika mzozo hausikilizwi: “Kama Mnyarwanda, hilo linaniudhi. Inaonekana kwamba nguvu fulani zinataka kuondoa uthabiti wetu. Nadhani jumuiya ya kimataifa lazima itambue ukweli ambao tunataka kushiriki.”
Leo Jumatatu Machi 17, 2025 mkutano wa Baraza la Umoja wa Ulaya unatarajiwa kuamua kuhusu vikwazo vinavyoweza kuwalenga watu wanaohusishwa na mashambulizi ya M23 yanayoungwa mkono na Rwanda mashariki mwa DRC.