
Mkuu wa zamani wa Kitivo cha Tiba cha Butare nchini Rwanda ameshtakiwa mjini Paris kwa mauaji ya halaiki, uhalifu dhidi ya binadamu na kula njama ya kutenda uhalifu huu.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Alphonse K., 74, ambaye ameishi Ufaransa kwa miaka 25, amewekwa chini ya usimamizi wa mahakama. Anashukiwa kushiriki katika mauaji ya halaiki ya Watutsi mwaka 1994 katikamkoa wa Butare.
Jina lake lilitajwa wakati wa kesi
Ikiwa uchunguzi ulifunguliwa Novemba 13, ni kwa sababu jina la Alphonse K. lilionekana huko Paris wakati wa kesi za Eugène Rwamucyo, daktari na mwalimu katika Chuo Kikuu cha Butare, aliyehukumiwa mwezi Oktoba mwaka uliyopita kifungo cha miaka 27 jela, na Sosthène Munyemana, daktari mwingine wa zamani wa Rwanda, ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 24 jela mnamo mwaka 2023.
Mkuu huyu wa zamani wa Kitivo cha Tiba huko Butare anashukiwa kuitisha mashambulizi dhidi ya Watutsi walio wachache wakati wa mkutano ulioandaliwa Mei 14, 1994 huko Butare, mbele ya Jean Kambanda, Waziri Mkuu wa serikali ya mpito wakati huo.
Siku hiyo, inadaiwa alitoa hotuba “ya mauaji ya halaiki” kama ile ya Kambanda, Mahakama ya Paris iliandika mnamo mwezi Desemba 2023 katika motisha ya hukumu iliyomtia hatiani Sosthene Munyemana. Kuna nakala ya matamshi yake, kulingana na shirika la habari la AFP. Alphonse K. pia anatuhumiwa kutoa maagizo ndani ya hospitali ya Butare yaliyolenga kuwaangamiza au kuwafukuza wagonjwa wa Kitutsi, wakimbizi au wafanyakazi.
Mashtaka yaliyofutiliwa mbali na wakili wake. “Hakuwahi kuwa na mtazamo huu na hakuwahi kutoa matamshi yaliyohusishwa naye,” anahakikisha wakili Marcel Ceccaldi, ambaye anaeleza kuwa mteja wake hakufunguliwa mashtaka na Mahakama ya Kimataifa ya Rwanda.