
Naibu msemaji wa serikali ya Rwanda Alain Mukuralinda alifariki Alhamisi, Aprili 3, katika hospitali ya Kigali kufuatia mshtuko wa moyo. Alikuwa na umri wa miaka 55.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Serikali ya Rwanda imethibitisha kifo cha naibu msemaji wake, Alain Mukuralinda, katika taarifa. “Tuna huzuni kubwa kutangaza kifo cha mwenzetu Alain Mukuralinda, Naibu Msemaji wa Serikali, katika Hospitali ya KFH kufuatia mshtuko wa moyo.”
Kiongozi mwenye uhusiano mzuri na vyombo vya habari vya Rwanda, Alain Mukuralinda amekuwa akishikilia wadhifa wa naibu msemaji wa serikali tangu mwezi Desemba 2021, anaripoti mwandishi wetu huko Kigali, Lucie Mouillaud. Nafasi ya pili baada ya msemaji mkuu Yolande, aliyeishikilia baada ya kuhudumu katika kitengo cha vyombo vya sheria. Baada ya kusomea sheria nchini Ubelgiji miaka ya 1990, alifanya kazi katika ofisi ya mwendesha mashtaka wa umma wa Rwanda kuanzia mwaka wa 2002…
Alain Mukuralinda, ambaye alikuwa msemaji wa ofisi ya mwendesha mashtaka na mwendesha mashtaka wa kitaifa, alishikilia baadhi ya nyadhifa za juu zaidi katika ofisi ya mashtaka ya Umma hadi mwaka wa 2015, akifanya kazi hasa katika kesi za madai ya mauaji ya kimbari na na kesi za viongozi mashuhuri wa kisiasa, ikiwa ni pamoja na kesi ya kiongozi wa upinzani Victoire Ingabire kati ya 2012 na 2013.
Mbali na kazi yake ya utumishi wa umma, Alain Muku, kama alivyokuwa akijulikana kwa jina la kikazi, alishika nafasi kubwa katika ulingo wa muziki wa nchi hiyo…hasa mtunzi wa wimbo uliokuja kuwa wimbo wa timu ya taifa ya kandanda ya Rwanda…