Ruto: Afrika inapoteza dola bilioni 18 kila mwaka kutokana na mizozo

Rais William Ruto wa Kenya ambaye yuko mstari wa mbele katika kupigania mageuzi ya kitaasisi ndani ya Umoja wa Afrika (AU), alisema jana Jumatatu kwamba mizozo inaendelea kuinyima Afrika uwezo wake na inalitia hasara kubwa bara hilo. Hasara hiyo inakadiriwa kufikia dola bilioni 18 kila mwaka na kuwafanya mamilioni ya Waafrika kuwa wakimbizi.