Russia yasisitiza umuhimu wa Mkataba wa Ushirikiano wa Kina wa Kistratejia na Iran

Dmitry Peskov, msemaji wa Ikulu ya Kremlin (makao makuu ya urais wa Russia), Jumanne alisema kuwa Russia inatilia umuhimu mkubwa kusainiwa mkataba wa ushirikiano wa kina wa kistratejia na Iran, akibainisha kuwa hatua hiyo ni sehemu muhimu sana ya safari ya Rais Masoud Pezeshkian wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini humo.