Russia: Kwa mtazamo wa mkuu wa UNICEF watoto wa Ghaza si muhimu kama wenzao wa Ukraine

Balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amemshutumu mkuu wa UNICEF kwa kuwapa kipaumbele watoto wa Ukraine kuliko watoto wenzao wa Ghaza baada ya kushindwa kulieleza Baraza la Usalama la umoja huo kuhusu masaibu ya watoto hao kama alivyofanya kwa watoto wa Ukraine.