
Ndege zisizokuwa na rubani kwa mara ya tano siku ya Alhamisi, zimeshambulia ngome za jeshi Mashariki na Kusini mwa nchi ya Sudan.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Mashambulio hayo yanatekelezwa na wanamgambo wa RSF wanaoendelea kupambana na jeshi, tangu mwezi Aprili 2023.
Mji wa Port Sudan, ambao umekuwa salama kipindi chote cha vita, na kuwa kimbilio kwa wakimbizi na makao makuu ya watoa misaada kwa watu waliothiriwa na vita.
Siku ya Alhamisi, mashambulio hayo yalilenga kambi ya jeshi la majini ya Flamingo, Kaskazini mwa Port Sudan.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress, ameonya kuwa iwapo mashambulio hayo yataendelea, maisha ya raia wa kawaida, yatakuwa hatarini na miundo mbinu muhimu itaharibiwa.
“Maisha ya raia wa kawaida, yapo hatarini na itatiza utoaji wa misaada ya kibinadamu,” Stephane Dujarric, msemaji wa Guteress, amesema.
Wanamgambo wa RSF wanaoripotiwa kutekeleza mashambulio hayo, hawajazungumzia kinachoendelea.
Vita nchini Sudan, vimesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwaacha watu wengine zaidi ya Milioni 13 bila makaazi, kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa.