
Vita na mashambulizi dhidi ya raia vinatarajiwa kuwalazimisha watu milioni 6.7 kutoka makwao duniani kote katika kipindi cha miaka miwili ijayo, Baraza la Wakimbizi la Denmark, Danish Refugee Council, (DRC) limesema leo Ijumaa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Hata hivyo, Danish Refugee Council (DRC) imesema hatua ya Marekani, Uingereza na Ujerumani ya ” kusiisha misaada ya kimataifa “imewanyima mamilioni ya watu walio hatarini msaada muhimu.
“Tunaishi katika zama za vita na kutokujali, na raia wanalipa gharama kubwa zaidi,” Katibu Mkuu wa shirika la Danish Refugee Council (DRC) Charlotte Slente amesema katika taarifa yake.
Idadi ya watu waliokimbia makazi yao duniani kote kwa sasa inafikia milioni 122.6, DRC imesema.
Shirika hilo limesema utabiri wake kuhusu kutoroka kwa raia makazi yao duniani ulionyesha “kuongezeka kwa idadi kubwa” kwa watu milioni 4.2 mnamo 2025, idadi kubwa zaidi iliyokadiriwa na DRC tangu mwaka 2021.
Tukio jipya la watu milioni 2.5 unatarajiwa mnamo mwaka 2026.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudani na Myanmar vitachangia karibu nusu ya watu wanaotarajiwa kuhama makwao.
Sudani
“Mgogoro wa dharura zaidi wa kibinadamu duniani” – utachangia karibu theluthi moja ya wakimbizi wapya, amesema, akibainisha kuwa watu milioni 12.6 tayari wameyakimbia makazi yao ndani ya Sudani na nchi jirani.
“Njaa imetumika kama silaha ya vita, ikisukuma nchi kutoka janga moja la njaa hadi lingine,” ripoti hiyo imesema.
Myanmar
Nchini Myanmar, vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyo na pande nyingi vimeongezeka, na kusababisha watu milioni 3.5 kuyahama makazi yao, na karibu watu milioni 20, au theluthi moja ya watu, wanahitaji msaada wa kibinadamu, DRC imesema.
Shirika hilo limetabiri kuwa nchi hiyo itashuhudia watu milioni 1.4 waliolazimika kuhama makazi yao ifikapo mwisho wa mwaka 2026.
Afghanistan, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Syria, Yemen na Venezuela pia zinatarajiwa kukumbwa na ongezeko la watu waliokimbia makazi yao kutokana na migogoro ya silaha, mabadiliko ya Tabianchi, matokeo ya vita na kuyumba kwa uchumi.
Kati ya watu milioni 6.7 wanaotarajiwa kuhama makazi yao mwishoni mwa mwaka 2026, karibu 70% watakuwa wakimbizi wa ndani, DRC inasema.
Bi Slente, kutoka shirika la Danish Refugee Council (DRC), amelaani uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump kufuta asilimia 83 ya programu za misaada ya kibinadamu ya USAID duniani kote, na kuutaja kuwa “usaliti kwa watu walio hatarini zaidi.”
“Tuko katikati ya hali mbaya duniani: idadi kubwa duniani ya watu wanaotoroka makazi yao, mahitaji yanayokua na upunguzaji mbaya wa bajeti,” amesema.
“Wafadhili wakuu wanaacha wajibu wao, na kuacha mamilioni ya watu katika mateso. Ni zaidi ya mgogoro. Ni kushindwa kimaadili. “