Rio: Amorim atapata kazi kusajili

Rio: Amorim atapata kazi kusajili

Manchester, England. Rio Ferdinand anaamini msimu wa hovyo wa Manchester United utawapa shida kwenye vita ya kusaka wachezaji wapya wa maana wa kuwasajili baada ya kichapo kutoka kwa Tottenham kwenye fainali ya Europa League na kupoteza tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Man United, inayoshika nafasi ya 16 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England ilimaliza ligi wikiendi hii, huku bao la Brennan Johnson walilofungwa kwenye fainali iliyofanyika Bilbao limempa presha kubwa kocha Ruben Amorim kwenye mpango wake wa usajili.

Ferdinand amesema: “Umekuwa msimu wa majanga ambao umemalizika vibaya sana, lakini nadhani walijitahidi sana. Kwenye ile fainali, kila timu ilikuwa inaogopa kupoteza.

“Huwezi kutarajia ushindi kama unacheza huku ukijinda, unakupaswa kuwa shupavu. Hii inafanya dirisha la usajili wa majira ya kiangazi kwenda kuwa refu sana.

“Wale wachezaji iliyokuwa inapiga hesabu kuwasajili wanapaswa kubadilika mipango kwa sababu hawapo tena kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mambo yatakuwa tofauti sana.”

Man United imekuwa ikihusishwa na mastaa kibao wa maana kwa ajili ya kuwaongeza kwenye kikosi chao, lakini sasa itakuwa ngumu kwao kuwapata kirahisi kutokana na kushindwa kuwapa fursa ya kucheza soka la Ulaya.

Timu hiyo imemaliza msimu ikiwa nafasi ya 16 ambayo ni mbaya zaidi kwao kwa kipindi cha hivi karibuni ikiwa haijatwaa kombe lolote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *