Reuters: RSF imetia saini hati ya kuunda serikali nyingine nchini Sudan

Wanasiasa wa Sudan, Al-Hadi Idris na Ibrahim Al-Mirghani, wameliambia shirika la habari la Reuters kwamba kundi la waasi la Rapid Support Forces (RSF) limetia saini mkataba na makundi washirika ya kisiasa na yenye silaha wa kuunda “serikali ya amani na umoja” sambamba na ile ya sasa nchini humo katika maeneo yanayodhibitiwa na kundi hilo.