
Kampuni ya kutengeneza magari ya Ufaransa ya Renault imetangaza siku ya Jumapili kwamba imewasiliana na Wizara ya Ulinzi kuhusu uwepo wake nchini Ukraine ili kuzalisha ndege zisizo na rubani kwa majeshi ya Ukraine na Ufaransa, lakini bado haijafanya “uamuzi wowote.”
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Tumewasiliana na Wizara ya Majeshi. Majadiliano yamefanyika, lakini hakuna uamuzi ambao umeidhinishwa kwa wakati huu kwa sababu tunasubiri ufafanuzi wa mradi huu kutoka kwa wizara,” Renault imeliambia shirika la habari la AFP.
Kulingana na Franceinfo, ambayo haikutoa maelezo ya vyanzo vyake, Renault na shirika la ulinzi la Ufaransa SME wanapanga kufungua njia za uzalishaji zinazopatikana “dazeni chache au mamia ya kilomita kutoka mstari wa mbele” huko Ukraine.
Taarifa hii inakuja siku mbili baada ya taarifa ya Waziri wa Ulinzi Sébastien Lecornu, akitangaza “ushirikiano ambao haujawahi kushuhudiwa kabisa ambapo kampuni kubwa inayozalisha magari ya Ufaransa (…) itaungana na shirika la ulinzi la Ufaransa la SME ili kuandaa njia za uzalishaji nchini Ukraine kuwa na uwezo wa kuzalisha ndege zisizo na rubani.”
Ndege hizi zisizo na rubani, ambazo mfano wake haujaainishwa, kimsingi zitahudumia jeshi la Ukraine, “lakini pia tutazishiriki na vikosi vyetu vya Ufaransa ili kuhakikisha mafunzo yanayoendelea ya kimbinu na uendeshaji ambayo yanaonyesha ukweli” wa mzozo wa Ukraine, Sébastien Lecornu alisema siku ya Ijumaa.
Ukraine inakusudia kutumia zaidi ya ndege zisizo na rubani milioni 4.5 kufikia mwaka 2025, ambazo zinahusika na 70% ya uharibifu wa vifaa vya adui kwenye mstari wa mbele.
Jeshi la Ufaransa, ambalo lina maelfu ya ndege zisizo na rubani, linatafuta kuokoa muda katika sekta hii.
Sébastien Lecornu anasma Waukraine “ni bora kuliko sisi katika uwezo wao wa kuunda drone na, juu ya yote, katika kuendeleza mafundisho yanayolingana.”
Pia watatoa maoni ya jinsi wanavyotumia ndege hizi zisizo na rubani katika vita hivi.