
Reli hii ilijengwa kuanzia mwaka 1970 na kukamilika mwaka 1975, ikiwa na urefu wa kilomita 1,860.5.
Reli hiyo imeanzia jijini Dar es Salaam, mji wa bandari nchini Tanzania na kwa upande wa Mashariki imeshia Kapiri Mposhi, katikati mwa Zambia kwa upande wa Magharibi.
Ujenzi wa reli hii ulilenga kuunganisha mikoa yenye shaba nchini Zambia na bandari moja kwa moja ili kusaidia Zambia ambayo haikupakana na bahari kujikita kiuchumi bila kutegemea Afrika Kusini na Zimbabwe.
Katika kipindi chote, reli hiyo ilisanifiwa kujengwa kwa uwezo wa kubeba metric tani milioni tano, lakini kutokana na sababu mbalimbali haikufikia lengo hilo.
Hata hivyo, kutokana na reli hiyo kujengwa miaka 50 iliyopita, kwa sasa imeharibika na kusababisha uwezo wake wa uendeshaji kupungua kwa kiasi kikubwa.
Kwa ajili ya kustawisha tena reli hii muhimu kimkakati, ukarabati wa kisasa umeonekana kuwa ni lazima ambao unahusiana na ufanisi wa usafirishaji wa rasilimali za madini, pia unaathiri maendeleo ya bandari nchini Tanzania.
Hivyo Desemba 2023, timu ya wataalamu kutoka nchini China ilifika Tanzania, ikafanya ukaguzi wa kina kuhusu uendeshaji na ufundi wake.
Baada ya utafiti wa kina, Februari mwaka 2024, upande wa China uliwasilisha mpango wa kuikarabati na kupanga kuuanzisha mradi huu kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta binafsi na umma (PPP) ili kukamilisha ukarabati wa kisasa wa reli.
Utiaji saini mkataba wa makubaliano (MoU) wa kuifanya kazi hiyo, ulifanyika wakati mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ulipofanyika Septemba 2024, mjini Beijing.
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Rais wa China, Xi Jinping na Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema, kwa pamoja walishuhudia hafla hiyo, makubaliano yalionyesha mwanzo wa ukarabati na ustawishaji wa reli hiyo.
Zipo faida mbalimbali zitakazopatikana baada ya ukarabati huo, ikiwemo kuongeza uwezo wa usafirishaji wa kila mwaka wa waendeshaji wote kwa wastani unaokadiriwa kutoka tani 50 hadi tani 200.
Pia, kutakuwa na nguvu kuu itakayokuza maendeleo ya kiuchumi nchini Tanzania na Zambia, kuongeza ajira, ujenzi wa miundombinu na maendeleo ya viwanda kwa jumla katika maeneo yaliyo karibu.
Aidha, kuna mazungumzo yanaendelea kati ya Kampuni ya Uhandisi na Ujenzi ya China (CCECC) na Tazara kupata kibali maalumu cha uendeshaji wa reli hiyo kwa miaka 30.
Kampuni hii inalenga kuanzisha ukarabati wa miundombinu na treni utakaochukua muda wa miaka miwili hivi baada ya makubaliano kutiwa saini.
Katika hatua nyingine, utunzaji wa historia ya kuanzishwa kwa reli hiyo, eneo la kumbukumbu ya Tazara lilifunguliwa rasmi katika Wilaya ya Chongwe, mkoani Lusaka, nchini Zambia.
Hii ni kutokana na wafanyakazi Wachina 36 waliopoteza maisha yao katika ujenzi wa reli hiyo waliozikwa katika eneo hilo, jambo ambalo linaashiria urafiki na ushirikiano wa kina baina ya China na Zambia.
Katibu Mkuu katika Wizara ya Utalii ya Zambia, Evans Muhanga, alieleza katika hafla ya uzinduzi kwamba alitumaini eneo hilo la kumbukumbu litawajulisha watu wengi zaidi wa Zambia historia ya ujenzi wa reli hiyo.
Pia, itakuwa ni sehemu ya kurithi urafiki kati ya China na Afrika, kwani hata mradi wa ufufuaji wa Reli ya Tazara si marudio ya historia tu, bali pia ni matarajio kwa siku zijazo.
Katika muktadha wa enzi mpya ya ushirikiano kati ya China na Afrika, reli hii itafufuliwa na kuwa ukanda unaounganisha mioyo ya watu wa China na Afrika.
Kupitia ujenzi wa Mpango wa “Ukanda na Njia” wenye ubora wa juu, kunalenga kukuza maendeleo ya kiuchumi ya kieneo na kuimarisha urafiki kati ya China na Afrika.
Pia, itasaidia kujenga jumuiya ya karibu zaidi ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja. Ufufuaji wake pia utakuza mawasiliano ya kieneo, pia utatia nguvu mpya katika Afrika na hata ushirikiano baina ya China na Afrika.
Tunaamini kwa dhati kwamba kupitia juhudi za pamoja, Reli ya Tazara itakuwa mandhari nzuri barani Afrika na kushuhudia historia tukufu ya ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika.
Song Yiting ni mwanafunzi wa shahada ya pili kutoka Chuo Kikuu cha Taaluma za Kimataifa cha Shanghai (SISU), anapatikana kwa baruapepe: [email protected]