Ratiba ya wakati na mahali yatapofanyika mazishi ya Shahidi Nasrullah na Shahidi Safiyyuddin yatangazwa

Kamati ya vyombo vya habari inayohusika na shughuli ya mazishi ya Katibu Mkuu na Mkuu wa Baraza la Kisiasa la Hizbullah ya Lebanon waliouawa shahidi imetangaza kuwa shughuli ya mazishi hayo itafanyika siku ya Jumapili, Februari 19 saa saba mchana.