Rais wa Zanzibar, Dkt

Rais wa Zanzibar, Dkt

Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi ametangaza dhamira ya Serikali ya kuifanya Pemba kuwa kitovu cha uwekezaji, biashara na maendeleo jumuishi yatakayowanufaisha wananchi wote.

Akiwahutubia wananchi na wawekezaji katika Tamasha la Uwekezaji Zanzibar 2025 lililozinduliwa leo katika Maeneo Huru ya Uwekezaji ya Maziwang’ombe, Mkoa wa Kaskazini Pemba, Rais Mwinyi alisema Serikali imejipanga kuhakikisha uwekezaji unakuwa chachu ya maendeleo ya kiuchumi kisiwani humo.

Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa Serikali inalenga kuvutia wawekezaji wa ndani na nje wenye maono ya muda mrefu, ili kuleta mabadiliko ya kweli kwa wananchi wa Pemba. Alisisitiza kuwa uwekezaji utakaowekwa utazingatia utoaji wa ajira kwa vijana, kuongeza pato la mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, sambamba na kukuza maendeleo endelevu yanayowagusa wananchi moja kwa moja.
Aidha, Rais Mwinyi ameeleza kuwa Serikali imepitisha sheria maalum inayowataka wawekezaji kushiriki katika huduma za kijamii kwenye maeneo wanayowekeza. Lengo la sheria hiyo ni kuhakikisha wananchi wa maeneo ya karibu na miradi ya uwekezaji wananufaika moja kwa moja kwa kupatiwa huduma kama elimu, afya na miundombinu bora.

Kufuatia mafanikio ya tamasha hilo, Rais Mwinyi alitangaza kuwa Tamasha la Uwekezaji litakuwa la kila mwaka, na kufuatia ratiba hiyo, Tamasha la Zanzibar Investment Summit 2026 litafanyika kisiwani Unguja. Hii ni ishara ya kujenga utamaduni wa kudumu wa kukuza uwekezaji visiwani Zanzibar kupitia ushirikishwaji wa sekta binafsi na wananchi.

#AzamTVUpdates
✍Mtumwa Said
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *