Rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz kufungwa miaka 20

Mwanasheria mkuu wa serikali huko Nouakchott nchini Mauritania ameomba kifungo cha miaka ishirini jela dhidi ya rais wa zamani wa nchi hiyo Mohamed Ould Abdel Aziz, anayetuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma na kujitajirisha kinyume na sheria katika kipindi chake cha uongozi. Adhabu hiyo inajiri baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano jela mwezi Desemba mwaka jana wakati wa kesi yake ya kwanza.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Rais wa zamani Mohamed Ould Abdel Aziz, ambaye aliongoza Mauritania kutoka mwaka 2008 hadi mwaka 2019, ameonekana pamoja na mawaziri wa zamani na maafisa kadhaa wakuu na viongozi wa makampuni. Wote wanatuhumiwa kwa “ushawishi wa biashara”, “utakatishaji wa pesa”, “matumizi mabaya ya majukumu” na “utajiri haramu”.

Utajiri wa Mohamed Ould Abdel Aziz unakadiriwa kuwa euro milioni 67. Kulingana na mwendesha mashtaka, nafasi ya mkuu wa zamani wa nchi ilimuwezesha, wakati huo, kutumia nafasi yake kuweka shinikizo kwa wawekezaji.

Hata hivyo, Mohamed Ould Abdel Aziz na mawakili wake wanakanusha shutuma hizi. Upande wa utetezi, ambao unatakiwa kuwasilisha hoja zake leo Jumanne mjini Nouakchott, umepinga taratibu za kisheria tangu kuanza kwa kesi hiyo. Kulingana na wao, ni Mahakama Kuu ya Mauritania pekee ndiyo yenye uwezo wa kumhukumu rais wa zamani.