Rais wa Sudan Kusini atoa amri ya kufanyika uchunguzi wa ajali ya ndege iliyoua watu 20

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini ameamuru uchunguzi ufanyike kuhusu ajali ya ndege iliyotokea jana Jumatano asubuhi na kusababisha vifo vya watu 20 wakiwemo raia wa kigeni katika Jimbo la Unity.