Rais wa Russia: Karibuni hivi viongozi wote wa Ulaya ‘watamtikisia mikia’ Trump japo hawampendi

Rais Vladimir Putin wa Russia amesema, Umoja wa Ulaya daima umekuwa ukipokea ishara za uchukuaji hatua zake za kisiasa kutoka Washington na utaendelea kufanya hivyo wakati huu Donald Trump akiwa madarakani; na kwamba licha ya baadhi ya viongozi wa umoja huo kupinga vikali kuchaguliwa tena Trump, rais huyo mpya wa Marekani “atarejesha utulivu” na utiifu wa EU “haraka sana”.