Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameapa vita ‘vikali’ vya kuwakomesha waasi wa M23

Rais wa Kongo Félix Tshisekedi ameapa kurejesha mamlaka ya serikali mashariki mwa nchi, ambako waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wameuteka mji wa Goma na wanaripotiwa kuelekea kusini kuchukua maeneo zaidi.