
Rais wa Ghana John Dramani Mahama alianza ziara yake siku ya Jumamosi, Machi 8, katika nchi tatu za Muungano wa Nchi za Sahel (AES) ambazo anataka kuzshawishi kujiunga tena na ECOWAS. Kwanza alikwenda Mali.
Imechapishwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu wa kikanda, Serge Daniel
Tangu kuchaguliwa kwake mwezi wa Desemba mwaka jana, John Dramani Mahama hajawahi kuficha nia yake ya kuona nchi tatu za Muungano wa Nchi za Sahel (Mali, Niger na Burkina) zikirejea katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi. Rais wa Ghana anakusudia kuchukua fursa ya ziara yake kuwasilisha ujumbe huu kwa viongozi watatu wa tawala za kijeshi: “Rudini kwa familia kubwa ya ECOWAS.”
John Dramani Mahama alianza ziara yake huko Bamako, ambapo kiongozi wa utawala wa kijeshi alikwenda uwanja wa ndege kumkaribisha. Mwisho wa siku, alitangaza kufanyika kwa Tume Kuu ya Pamoja ya Ushirikiano wa Mali-Ghana. Rais wa Ghana pia alisema kuwa bandari za nchi yake tayari zinapatikana kwa Mali, ambayo haina sehemu ya mbele ya bahari. Ofa yake pia inatumika kwa Niger na Burkina Faso.
Kuondoka kwa nchi tatu za ECOWAS ilikuwa mada nyingine ya majadiliano. John Dramani Mahama akimsikiliza kwa makini kiongozi wa utawala wa kijeshi wa eneo hilo kuhusu mada hiyo. “Lazima kuwe na kiwango cha chini cha kuheshimiana kati ya ECOWAS na nchi tatu za AES,” rais wa Ghana aliwaambia waandishi wa habari. Aliongeza: “Kutokuwa na imani ndio chanzo cha mifarakano, lakini tunaamini kwamba bado inawezekana kupata muafaka.”
Wakati huo huo, John Dramani Mahama ni mtetezi mkubwa wa kuboresha uhusiano kati ya nchi tatu zinazoongozwa na wanajeshi waliofanya mapinduzi na ECOWAS. Mamlaka ya Mali, Burkina Faso na Niger zinategemea hasa ushirikiano mzuri kati ya AES na ECOWAS katika suala la usafirishaji huru wa bidhaa na watu. Kwa mujibu wa mjumbe wa ujumbe wa Ghana, mazungumzo hayo pia yatajadili mapambano dhidi ya ugaidi katika kanda hiyo. Katika eneo hili, Ghana inafanya majaribio ya mkakati unaoitwa “Accra Initiative” ambao ni tofauti na ule wa ECOWAS.