Rais wa Colombia alegeza kamba baada ya Trump kuamuru vikwazo dhidi ya nchi hiyo

Rais Donald Trump wa Marekani jana alisema kuwa ataiwekea Colombia ushuru wa asilimia 25 na vikwazo baada ya nchi hiyo ya Amerika ya Kusini kukataa kuruhusu kutua nchini humo ndege mbili za kijeshi za Marekani zilizobeba wahamiaji waliofukuzwa huko Marekani.