Rais wa Afrika Kusini na Trump kukutana wiki ijayo White House

Rais wa Marekani Donald Trump na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa watakutana katika Ikulu ya White House wiki ijayo kufuatia madai ya Trump – yaliyokanushwa na Afrika Kusini – kwamba “mauaji ya halaiki” yanafanywa dhidi ya wakulima wa kizungu katika nchi hiyo yenye watu wengi weusi.

Imechapishwa:

Dakika 3

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo uliotangazwa siku ya Jumatano na serikali ya Afrika Kusini na uliopangwa kufanyika Mei 21, pia unakuja baada ya Marekani kuwakubali Waafrika Kusini weupe 59 kama wakimbizi siku ya Jumatatu. Mapokezi hayo yanaashiria mwanzo wa kile ambacho serikali ya Trump inakitaja kama mpango mkubwa wa kuwahamisha wakulima wachache wa Kiafrikana, ambao Trump anasema wameteswa katika nchi yao kwa sababu ya asili yao ya kikabila. Afrika Kusini inakanusha madai hayo na kusema watu weupe katika nchi hiyo yenye watu weusi wengi hawateswi.

Ofisi ya Bw Ramaphosa imesema atakuwa Marekani kuanzia Jumatatu hadi Alhamisi wiki ijayo na atakutana na Bw Trump katika Ikulu ya Marekani siku ya Jumatano. Ziara ya Ramaphosa ingelenga “kuweka upya uhusiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili,” ofisi yake imesema.

Ikulu ya White House imekataa kutoa maoni yake mara moja kuhusu mkutano huo, ambao ni wa kwanza kwa Trump kuwa na kiongozi wa taifa la Afrika tangu arejee madarakani mwezi Januari.

Trump ameikosoa serikali ya Afrika Kusini inayoongozwa na watu weusi katika nyanja kadhaa na kutoa agizo la kiutendaji mnamo Februari 7 kukata ufadhili wote wa Marekani kwa nchi hiyo kama adhabu kwa kile alichokiita sera za ndani dhidi ya watu weupe na sera za kigeni dhidi ya Marekani.

Rais huyo wa chama cha Republican ameibainisha Afrika Kusini kwa kile Marekani inachokiita sheria za kibaguzi dhidi ya watu weupe na kuishutumu serikali kwa “kuchochea” vurugu dhidi ya wakulima wa kizungu. Serikali ya Afrika Kusini inasema idadi ndogo ya mauaji ya wakulima wa kizungu inapaswa kulaaniwa, lakini kwamba ni sehemu ya matatizo ya uhalifu wa kikatili nchini humo na hayana msukumo wa ubaguzi wa rangi.

Trump ametangaza siku ya Jumatatu – siku hiyo ambayo kundi la kwanza la wakimbizi wa Kiafrikana liliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dulles huko Virginia – kwamba “mauaji ya halaiki” dhidi ya wakulima wa kizungu yalikuwa yanaendelea, jambo ambalo lilipuuzwa na vyombo vya habari vya kimataifa.

Ukosoaji wa Marekani kwa kile wanachokiita sheria za kibaguzi na dhidi ya Wazungu wa Afrika Kusini unaonekana kurejelea sheria za Afrika Kusini za upendeleo ambazo zinakuza fursa kwa watu Weusi, pamoja na sheria mpya ya unyakuzi wa ardhi ambayo inaruhusu serikali kunyakua ardhi ya kibinafsi bila kulipwa fidia. Ingawa serikali inadai kuwa sheria ya ardhi sio chombo cha kunyang’anya ardhi na inalenga ardhi isiyotumika ambayo inaweza kugawanywa kwa manufaa ya umma, baadhi ya makundi ya Kiafrikana yanasema inaweza kuruhusu ardhi yao kunyakuliwa na kugawanywa kwa sehemu ya weusi walio wengi nchini humo.

Tangu arejee afisini mwezi Januari, Trump ameagizwa kukomeshwa kwa programu tofauti, usawa na ushirikishwaji ndani ya serikali ya shirikisho. Utawala pia ulitishia taasisi zisizo za kiserikali kama vile vyuo na vyuo vikuu kupoteza misaada yao ya kifedha ikiwa hazitafanya vivyo hivyo.

Trump pia aliwataka wanakandarasi wa serikali na wapokeaji wengine wa fedha za shirikisho kuthibitisha, chini ya tishio la adhabu kali za kifedha, kwamba hawatendi programu za DEI kwa kukiuka sheria za kupinga ubaguzi.

Waafrikna ni wazao wa walowezi, hasa Waholanzi, Wafaransa na Wajerumani, waliofika Afrika Kusini katika karne ya 17. Walikuwa viongozi wa mfumo wa awali wa nchi wa ubaguzi wa rangi. Kuna takriban Waafrikana milioni 2.7 kati ya wakazi milioni 62, zaidi ya 80% kati yao ni watu weusi. Pia kuna karibu watu wengine milioni 2 wazunu wenye asili ya Uingereza na asili nyingine.

Trump pia aliishutumu Afrika Kusini kwa kuchukua “misimamo ya uchokozi kuelekea Marekani na washirika wake” katika sera yake ya nje na kuunga mkono Hamas, kundi la wanamgambo wa Palestina na Iran.

Agizo la kiutendaji la Trump linautaja uamuzi wa Afrika Kusini wa kumshutumu mshirika wa Marekani Israeli kwa mauaji ya halaiki huko Gaza katika kesi inayoendelea mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki kama mfano wa msimamo wake dhidi ya Marekani. Israeli ilifanya mashambulizi ya kijeshi huko Gaza baada ya wanamgambo wa Hamas kuua watu 1,200 wakati wa uvamizi kusini mwa Israeli mnamo mwezi Oktoba 2023.

Operesheni hiyo ya Israel iliua zaidi ya Wapalestina 52,928 wengi wao wakiwa wanawake na watoto, kwa mujibu wa wizara ya Afya inayoongozwa na Hamas.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *