
Kufuatia matukio ya hivi punde mashariki mwa DRC na kusonga mbele kwa waasi wa AFC/M23 wakiungwa mkono na wanajeshi wa Rwanda kuelekea mkoa wa Kivu Kusini, kwa mujibu wa mamlaka ya Kongo, Rais Félix Tshisekedi amekatisha ziara yake nchini Ujerumani siku ya Ijumaa tarehe 14 Februari na hivyo kurejea Kinshasa. Hatahudhuria mkutano wa kilele wa Umoja wa Afrika, AU, mjini Addis Ababa kama ilivyopangwa awali, kwa mujibu wa ofisi ya rais wa Kongo.
Imechapishwa:
Dakika 2
Matangazo ya kibiashara
Rais wa Kongo amejibu siku ya Ijumaa kuhusu wapiganaji wa AFC/M23 na washirika wao Rwanda ambao wanaendelea kusonga mbele katika mkoa wa Kivu Kusini. Wakati wa mchana, wapiganaji wa M23 walidhibiti uwanja wa ndege wa Kavumu, karibu kilomita thelathini kutoka Bukavu. Jioni, chanzo cha serikali kimeongeza kuwa wapiganaji wa M23 sasa wanaripotiwa katika jiji la Bukavu.
Kutoka Munich, ambako alikuwa akishiriki katika mkutano wa kimataifa wa usalama, Félix Tshisekedi hakutoa maoni moja kwa moja juu ya maendeleo ya hivi punde yawaasi wa AFC/M23 . Lakini bado anashikilia msimamo wake: “Hakuna mazungumzo na AFC/M23.” Mkuu wa nchi anashutumu “nia” ya Rwanda ya kupanua nchi yake kwa kuingia DRC. RaisTshisekedi amesema, ni haraka kuchukua hatua.
Leo hatutarajii maneno tu, tunataka hatua madhubuti. Hali ilivyo ni udanganyifu. Kwa kutofanya chochote basi ni chaguo. Na chaguo hili, ikiwa litaendelea, litakuwa na athari mbali zaidi ya mipaka ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kwani tukiruhusu nchi moja kuchora upya mipaka ya Afrika kwa nguvu leo, nani atafuata? Je! ni eneo gani litakalofuata kwa kupinga hili? Ni taifa gani litakalopata madhara ya mfano huu hatari? Ni wakati wa kuchukuwa hatua. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni nchi huru na kama nchi yoyote huru, ina haki na wajibu wa kulinda uadilifu wa eneo lake na kulinda watu wake. Kutokana na uchokozi tunaofanyiwa, tutatumia kila njia ili kurejesha amani na kudhamini usalama wa taifa letu. Hatutakubali tena kwamba nchi yetu inatumika kama uwanja wa vita kwa matamanio ya kikatili ya baadhi ya majirani zetu. Hatutavumilia tena rasilimali zetu za kimkakati kuporwa kwa manufaa ya maslahi ya kigeni chini ya macho ya wale wanaochochea machafuko.
Rais Félix Tshisekedi anasema kundi hili lenye silaha “ni sanamu tu ambalo Rwanda inaweka mbele, lakini nyuma yake, ni jeshi la Rwanda ambalo linaongoza mapigano. “
Rais wa Kongo anaenda mbali zaidi na kumshutumu moja kwa moja mtangulizi wake, Joseph Kabila, kuhusika na upinzani wenye silaha. “Mfadhili halisi wa upinzani huu ni mtangulizi wangu, Joseph Kabila. Lakini hakiri hili, hakubali matendo yake. “