Rais Tshisekedi aapa kuendesha vita ‘vikali’ vya kuwakomesha waasi wa M23

Rais Félix Tshisekedi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ameapa kurejesha mamlaka ya serikali mashariki mwa nchi, ambako waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wameuteka mji wa Goma na wanaripotiwa kuelekea kusini kuchukua maeneo zaidi.