Rais Donald Trump amewasili nchini Saudi Arabia akianza ziara yake katika mataifa ya Ghuba ambapo atazuru pia Qatar katika juhudi za kufanikisha makubaliano ya kibiashara.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1
Matangazo ya kibiashara
Trump ambaye ameandamana na Waziri wake wa mamabo ya kigeni Marco Rubio, tayari amekutana na Mwanamfalme Mohammed bin Salm.
Hii ndio ziara kubwa ya rais Trump nje ya nchi katika muhula wake wa pili ofisini, White House ikisema inatazamia kurejea kihistoria katika eneo hilo.
Miaka minane iliopita, rais Trump pia alichagua Saudi Arabia kwa ziara yake ya kwanza nje ya nchi.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema hatua ya Trump kuzuru eneo hilo lenye utajiri wa mafuta, inaonyesha umuhimu wa eneo hilo kwa Marekani.
Baadaye rais Trump anatarajiwa kuzuru pia nchi ya Qatar baada yake kuhudhuria mkutano wa viongozi wa mataifa ya Ghuba.
Kuelekea ziara hii, White House imeonekana kuchangia pakubwa katika kupatikana kwa utulivu kati ya mataifa ya India na Pakistan, kuachiwa kwa raia wa Marekani aliyekuwa anazuiliwa Gaza pamoja na kufanya mazungumzo mengine kuhusu silaha za nyukilia na Iran.