Rais Trump akerwa na Putin kuhusiana na mazungumzo na Ukraine

Rais wa Marekani, Donald Trump, hapo jana amewasuta rais wa Urusi, Vladimir Putin na mwenzake wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, wakati huu juhudi za kuanza mazungumzo ya kusitisha mapigano zikiendelea kukwama.

Imechapishwa:

Dakika 1

Matangazo ya kibiashara

Mwanzo, rais Trump ameelezea kughdhabishwa na rais Putin ambapo amemkosoa kwa kutilia shaka uaminifu wa rais Zelensky kama mshirika katika mazungumzo hayo.

Baada ya kumsuta Putin, Trump alimgeukia rais Zelensky, akimuonya kuwa Ukraine itapata matatizo makubwa iwapo atajiondoa kwenye makubaliano kuhusu kuipa Marekani haki ya kipekee juu ya madini ya Ukraine.

Tangu kurejea madarakani, Trump amekuwa kijaribu kusuluhisha mzozo wa Ukraine kupitia makubaliano ya usitishaji mapigano kati ya Ukraine na Urusi, lakini utawala wake umeshindwa kufikia makubaliano licha ya majadiliano na pande zote.

Donald Trump, amekuwa akishinikiza kupatiakana kwa mwafaka kati ya rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine na Vladimir Putin wa Urusi.
Donald Trump, amekuwa akishinikiza kupatiakana kwa mwafaka kati ya rais Volodymyr Zelensky wa Ukraine na Vladimir Putin wa Urusi. AFP – JIM WATSON,JOHN THYS,EVGENIA NOVOZHENINA

Katika hatua nyingine Putin, alikataa pendekezo lamarekani la kusitisha vita kwa siku 30, na badala yake kupendekeza rais Zelensky kuondolewa ofisini kama sehemu ya mchakato wa amani.

Naye Zelensky, amemshtumu Putin kwa kukwamisha mazungumzo, huku akiwa hana nia ya kusitisha mashambulio yake katika rdhi ya Ukraine.

Haya yanajiri wakati Urusi ikiendeleza mashambulio yake katika ardhi ya Ukraine, ambapo hapo jana vikosi vya Moscow vimeteka kijiji cha Dnipropetrovsk

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *